Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1,
2013 akisalimiana na Mama Rachel Chebet, mke wa Naibu Rais mteule wa
Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akiongea na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1,
2013 akimuongoza kuelekea kwenye chakula cha mchana Naibu Rais mteule
wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto na mkewe Rachel Chebet katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akipozi na familia ya Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ya Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
PICHA NA IKULU
============================== =
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS
KIKWETE AKUTANA NA NAIBU RAIS WA KENYA
WILLIAM RUTO MBUGANI SERENGETI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya
Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 amekutana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe. William
Kipchirchir Samoei arap Ruto ambaye
alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Akiongea na mgeni huyo katika hoteli ya Kitalii ya
Seronera iliyoko katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani
Mara, Rais Kikwete amempongeza
Mhe Ruto na Rais mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, kwa ushindi wao kwenye
uchaguzi mkuu nchini Kenya.
Mhe Rais pia alimuelezea Mhe Rutto juu ya furaha yake pamoja na kuridhishwa na jinsi
uchaguzi ulivyofanyika kwa amani katika nchi hiyo.
Alielelezea
matumaini yake ya kuwa urafiki
uliopo kati ya Tanzania na Kenya
utadumishwa pamoja na kusukuma
mbele gurudumu la maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhe Rutto, ambaye aliwasili mkoani Mara wiki
iliyopita akiwa na mke wake na watoto, ameondoka leo baada ya chakula cha mchana alichoandaliwa
na mwenyeji wake.
Mwisho
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
1 Aprili,
2013
0 comments:
Post a Comment