TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bibi
Juliet Rugeiyamu Kairuki kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC).
Taarifa
iliyotolewa leo, Jumatatu, 22 Aprili, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu
Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Aprili
12, mwaka huu, 2013.
Bibi
Kairuki ni Mwanasheria mwenye Shahada ya Kwanza na ya Uzamili kwenye sheria. Ni
mtaalam wa miradi ya ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partnership). Kati ya
mwaka 2002 na 2008 alikuwa Meneja wa Mradi wa Public Private Partnership Capacity Building in SADC, katika Chama
cha Mabenki ya Afrika Kusini (The Banking
Association South Africa). Kuanzia mwaka 2008 hadi sasa Bibi Kairuki ni
Meneja Mkuu wa Idara ya Benki na Huduma za Fedha katika taasisi hiyo.
“Mwisho”
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR
ES SALAAM.
22
Aprili, 2013
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment