
Aliyekuwa
Mhasibu katika ofisi ya Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali, Godfrey Mbwilo
(katikati) akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi akipelekwa kizimbani kwa
tuhuma za wizi wa Sh150 milioni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es
Salaam jana. Picha na Venance Nestory.
Aliyekuwa mfanyakazi wa
Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Godfrey Mbwilo amefikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na tuhuma za wizi wa Sh153
milioni.
Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi,
Augustina Mmbando, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumain Kweka alidai kuwa
mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka hayo juzi mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando
na Wakili wa Serikali Tumaini Kweka alidai kuwa mshtakiwa alifanya makosa hayo
kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu.
Kweka alidai kuwa Agosti 2, 2011 katika ofisi za
Mkemia Mkuu wa Serikali, akiwa mtumishi wa umma aliiba Sh40 milioni mali ya
Serikali zilizofika kwake kulingana na nafasi yake ya ajira.
Katika shtaka la pili, Kweka alidai kuwa Septemba 5,mwaka huo katika ofisi hizo aliiba Sh45 milioni mali ya Serikali zilizofika kwake kulingana na nafasi yake ya ajira.
Via: Dj Sek
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment