WAZIRI MKUU,
Mizengo Pinda
WAZIRI MKUU,
Mizengo Pinda ameongoza harambee ya papo kwa papo na kufanikiwa kukusanya sh. milioni 31.5 zikiwa ni ahadi na fedha taslimu kwa
ajili ya ukarabati wa Kanisa Katoliki la Mashahidi wa Uganda la Magomeni,
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na
waumini wa Kanisa hilo leo asubuhi (Jumapili, Machi 17, 2013) kabla ya
kuendesha harambee hiyo, Waziri Mkuu aliusifu uongozi wa Kanisa Katoliki la
Magomeni kwa kuamua kufanya upanuzi wa kanisa hilo ili liweze kuhudumia waumini
wengi zaidi.
“Nia yao ni nzuri
sana na wameona mbali mapema. Magomeni hii ya
leo si ya wakati ule, na wala haitakuwa hivi katika miaka mingine 50 ijayo.
Zamani usingeweza kuona hata ghorofa moja hapa Magomeni lakini sasa hivi
maghorofa hayahesabiki,” alisema.
Aliwasisitiza
waumini hao kujitoa kwa ajili ya kazi ya Bwana kwa sababu hakuna sadaka ambayo
ni ndogo. “Hakuna sadaka iliyo ndogo mbele ya Mungu, kikubwa ni
dhamira tu. Kanisa ni letu na litajengwa na sisi waumini ili mradi kila mmoja
wetu aseme Kansa hili nitalijenga,” alisisitiza.
Mapema
akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na waumini hao, Baba Paroko wa kanisa
hilo, Padri Sixfrious Rwechungura alisema wameanza kazi ya ukarabati tangu
Agosti 15, 2011 na kwamba hadi sasa wamekwishakusanya sh. milioni 350
iliyotokana na nguvu za waumini wenyewe bila msaada wa kutoka nje.
Alisema wanahitaji
kiasi cha sh. milioni 300 ili kukamilisha kazi hiyo ambayo inapaswa kukamilika
katika miaka miwili ijayo ili iendane na maadhimisho ya miaka 50 ya kanisa
hilo.
0 comments:
Post a Comment