Wakulima wa bonde la Mpunga
Kiwalani Mlandizi mkoani Pwani wamelalamikia hatua ya halmashauri ya Kibaha
Vijijini kuchukua eneo lao bila maridhiano na kulibadilisha matumizi yake.
Mwenyekiti wa umoja wa wakulima
hao Rajab Chuma amesema utaratibu wa kuwaondoa katika eneo la Kiwalani
haukushirikisha pande zote mbili ili kufikia muafaka kabla ya kubadilisha
matumizi ya ardhi ambalo awali lilitumika kwa ajili ya kilimo.
Mwenyekiti huyo amesema chanzo
cha mgogoro huo ni mkuu wa shule ya sekondari na halmashauri kutaka kuwahamisha
kwa madai kwamba ni wavamizi kitu ambacho kimewashangaza kwani walimiliki
maeneo hayo hata kabla ya sekondari kujengwa.
Katibu wa umoja wa wakulima hao
Abillahi Rashidi Saad amesema
kuwa wanapanga kwenda mahakamani na kulifikisha suala hilo kwa waziri wa
ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi ili kupata suluhu ya tatizo hilo.
Hata hivyo Mkurugenzi hakuweza
kupatikana ili kutoa ufafanuzi juu ya
suala huku Mkuu wa Shule ya Sekondari
Ruvu kutopatikana kwa madai ya ya kuwa
nje ya kituo chake kwa shughuli maalum ya kikazi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment