Naibu waziri
wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu
Watanzania wametakiwa kuendelea kufanya jitihada
za makusudi katika kutunza miti ili uhifadhi
wa mazingira kwa ustawi wa jamii kwa
ujumla.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Mbao
ya miti ulimwenguni,ambayo kitaifa imefanyika jijini Dar es Salaam,Naibu waziri
wa Mali Asili na Utalii Lazaro Nyalandu amesema miti ni muhimu kama rasilimali.
Serikali imesema itaendelea kutunza mazingira ya
Tanzania kwa kukomesha ukataji miti na misitu bila vibali kwani vitendo hivyo
ni kinyume cha sheria.
Naibu Waziri huyo amesema watanzania wanatakiwa
kuendelea kupanda na kutunza miti iliyopo kwani husaidia kuleta mvua za kadiri
na kuzuia nchi kugeuka Jangwa.
Hata hivyo alizungumzia bidhaa zinazotokana na
Mbao amesema kazi za ubunifu kama uchongaji vinyago ni muhimu kama ajira na
biashara lakini kwa wahusika wafanye kazi kwa kufuata sheria.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment