Taasisi ya tuzo ya wanawake wenye mafanikio Tanzania TWAA imewataka wanawake kuwa na mtazamo chanya na kuonesha mchango wao katika jamii.


Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Sadaka Gandi amesema lengo siyo kushindana katika utoaji wa tuzo bali ni kuonesha mchango wa mwanamke na mafanikio katika jamii.

Mwenyekiti huyo amesema wanawake hawatakiwi kujiweka nyuma kwani TWAA wanachokifanya ni kuwashirikisha na kuwaonesha wanawake wengine kutambua mchango wao katika jamii.

TWAA kwa mwaka huu imepata washiriki 530 kutoka Tanzania nzima ambapo tarehe 28 mwezi huu huu atapatikana mshindi wa tuzo husika.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top