Waalimu wote ambao walikuwa wameajiriwa na serikali kabla ya kwenda masomoni na kufanikiwa kufaulu mafunzo yao mwaka 2012 katika ngazi za shahada na tashahada wametakiwa kurudi katika vituo vyao vya kazi.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliendelea kusema kuwa, kwa waalimu waliopangiwa vituo vipya vya kazi kimakosa wanpaswa kuripoti katika vituo vyao vya awali walivyopangiwa kabla ya kwenda masomoni.

Chanzo:Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top