BARAZA LA MITIHANI LA
TANZANIA
LIMEONGEZA
MUDA WA KUJISAJILI KWA WATAHINIWA WA KUJITEGEMEA CSEE NA QT 2013
KATIBU MTENDAJI BARAZA
LA MITIHANI LA TANZANIA ANAPENDA KUWATANGAZIA WATU WOTE WANAOKUSUDIA KUFANYA
MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) KAMA
WATAHINIWA WA KUJITEGEMEA NA MTIHANI WA MAARIFA (QT), KWAMBA MWISHO WA KIPINDI CHA USAJILI UMEONGEZWA KUTOKA TAREHE
28/02/2013 HADI TAREHE 31/03/2013 KWA USAJILI WA MALIPO YA
KAWAIDA (SHILINGI 35,000/- KIDATO
CHA NNE NA SHILINGI 20,000/- MTIHANI
WA MAARIFA-QT).
AIDHA KIPINDI CHA
USAJILI WA MALIPO PAMOJA NA FAINI KIMEONGEZWA KUTOKA TAREHE 1 APRILI 2013 HADI TAREHE 30 APRILI 2013. KATIKA KIPINDI HIKI, WAOMBAJI WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE WATAJISAJILI KWA ADA YA
SHILINGI 50,000/- (ADA PAMOJA NA
FAINI) NA WAOMBAJI WA MTIHANI WA MAARIFA (QT) WATALIPA SHILINGI 30,000/- (ADA PAMOJA NA FAINI).
WAOMBAJI WOTE
WATAJISAJILI KWA NJIA YA MTANDAO KUPITIA TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI YA: www.necta.go.tz.
IMETOLEWA
NA:
KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
CHANZO: Baraza la Mitihani Tanzania
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment