Mwenyekiti wa Baraza la Habari la Kiislam Tanzania BAHAKITA,Sheikh Said Mwaipopo (kushoto) akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na suala la mgogoro wa gesi  kusafirishwa kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Anayefuata ni katibu wa Chifu Hussein Msopa.
   Afisa habari wa Baraza la Habari la Kiislam Tanzania BAHAKITA,Sadiki Godigodi akifafanua jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na suala la mgogoro wa gesi  kusafirishwa kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Wanasiasa wametakiwa kutolifanya suala la gesi Mtwara kuwa mtaji wa kisiasa kwani suala hilo linaweza kuigawa nchi vipande vipande na kuhatarisha umoja amani na mshikamano ambao ulijengwa na waasisi wa  Taifa hili.

Mwenyekiti wa Baraza la Habari la Kiislam Tanzania BAHAKITA Sheikh Said Mwaipopo amesema kauli za wanasiasa mufilisi zinaipotosha jamii kwa maslahi binafsi huku wakijua ukweli kuwa suala la rasilimali nchini ni la Watanzania wote.

Mwenyekiti huyo amesema kuna mazingira ambayo hata wanachama wa chama tawala CCM walifikia hatua ya kutofautiana na msimamo wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kitu ambacho amedai ni hatari kwa ustawi wa taifa hili.

Akitoa tamko mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu mkuu wa baraza hilo Chifu Hussein Msopa amesema kuwa masuala wanasiasa na viongozi wa dini kushabikia vurugu za kudai rasilimali unaweza kuligawa Taifa kwa Misingi ya ukanda .

Katibu huyo amesema kuwa suala la gesi ni la kiuchumi zaidi ambalo linahitajika utaalam hivyo baraza lake linashauri kuwa mipango na mikakati ya maendeleo kwa wananchi inatakiwa kufafanuliwa na wananchi kuelimishwa mapema ili kuepuka vurugu zisizo za lazima.

Baraza hilo limeipongeza serikali kwa kuweza kuwasikiliza wananchi wa Mtwara na Lindi na kujua kero zinazowakabili na kuwashauri kutekeleza ahadi ambazo waziri mkuu Mizengo Pinda alizitoa wakati wa usuluhishi wa mgogoro hivi karibuni.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top