Tume ya nguvu za atomiki nchini imewataka wananchi wasiwe na hofu ya Tanzania kuwa na kinu cha nyuklia nchini ambacho kitasaidia na kurahisisha shughuli mbalimbali za kijamii kama vile tiba na afya, ujenzi, viwanda, kilimo pamoja na mifugo.
 
Akiongea katika kongamano lililoandaliwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa waandishi wa habari nchini, mkurugenzi wa tume ya atomiki Professa Idd Mkilaha amesema kuwa ni wakati sasa wa wananchi kuondokana na hofu juu ya matumizi ya madini ya uranium ambayo hutumika kutengeneza nyuklia.
 
Profesa Mkilaha amekanusha madai ya watu kuathirika na madini ya uranium katika maeneo mbalimbali ambako madini hayo yanapatikana na kusema kuwa huo ni uvumi na uchochezi unaofanywa na watu wachache kwani tume yake ilifanya uchunguzi kuhusiana na madai hayo lakini hakukuwa na ukweli wowote.
 
Toka madini hayo ya uranium yagunduliwe nchini, wanaharakati mbalimbali ndani na nje ya nchi wamekuwa wakiitaka serikali kusitisha uchimbaji wake kutokana athari zinazosababishwa na madini hayo yanayopatikana kwa wingi katika nchi ya Australia.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top