Waziri Hussein Mwinyi akipata maelekezo kutoka kwa kamishina wa wizara ya Afya juu ya vifaa walivyokabidhi kwa watu wenye ulemavu vikiwemo viti na bajaji kwa ajili ya kuwasaidia kujongea.
Kessy Abdallah Fundikira akijaribu bajaji yake huku akiongea mara baada ya kukabidhiwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii
 
Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetoa vifaa mbalimbali vya kuwawezesha wazee na watu wenye ulemavu kujongea kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa urahisi zaidi.
Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii Dakta Hussein Mwinyi amevitaja baadhi ya vifaa hivyo ni pamoja na  bajaji 10,vitanda 117,mashuka , mablanketi,magodoro zaidi ya  elfu moja ,viti 30 na kompyuta  10 maalum kwa watu wenye ulemavu vyote vikiwa na thamani ya milioni 500.
 
Dakta Mwinyi amewataka wanufaika wa vifaa hivyo kuvitumia kwa uangalifu kwani serikali bado inajitahidi kuwafikia watu wengine wenye mahitaji mbalimbali hapa nchini lakini kutokana na ufinyu wa bajeti wanalazimika kutoa misaada hiyo kwa awamu.
 
Nao wanufaika wa msaada  huo Mzee Kssy Abdallah Fundikira na Elisante Msabaha wamesema  msaada huo umekuja wakati muafaka na kuziomba wizara, idara , sekta na watu  binafsi kuwasaidia watu wenye makundi maalum wakiwemo walemavu na watoto kwa mahitaji mbalimbali.
 
Waziri mwinyi amesema  mwongozo wa kuwatambua watoto wenye ulemavu umeandaliwa ili  kuweza kuwapa huduma stahiki wangali wadogo kwa ukaribu zaidi na kustawisha maendeleo yao.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top