Waislam wametakiwa kuwa na subira na kufuata sheria za nchi wanapotakiwa kutimiziwa madai yao mbalimbali yanayohusiana na dini yao badala ya kutumia njia ya maandamano ambayo yaweza kuzusha machafuko hapa nchini.
 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Islamic Peace Foundation Sadick Godigodi amesema suala la maandamano linatakiwa kutumika baada ya jitihada zote za majadiliano na kisheria kushindikana.
 
Bwana Godigodi amesema suala la dhamana  ya Sheikh Ponda  Issa Ponda ambaye yuko  rumande ni suala la kisheria zaidi hivyo inatakiwa kuacha mhimili wa mahakama kutimiza wajibu wake badala ya kutumia maandamano kushinikiza kitu ambacho amedai si sahihi kwa nchi inayofuata utawala
wa sheria.
 
Baadhi ya makundi ya Kiislam yalipanga kufanya maandamano leo  Ijumaa kushinikiza mahakama kumpatia dhamana Sheikh Issa Ponda ambaye anatuhumiwa kwa uchochezi wa wananchi dhidi ya Serikali.
 
Tayari jeshi la Polisi kupitia kwa Kamanda Msaidizi Ahmed Msangi  wa kanda maalum Dar es Salaam iliwaagiza wananchi na waislam kwa ujumla kutofanya maandamano kwani wanaweza kuingilia uhuru wa utendaji wa mahakama.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top