Wito umetolewa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu katika hospitali na vituo vya afya ili kuokoa maelfu ya Watanzania wanaohitaji kuongezewa damu katika sehemu mbalimbali hapa nchini.

Afisa uhamasishaji kutoka mpango wa Taifa wa Damu Salama,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Desteria Nanyanga amesema kuwa Watanzania wanatakiwa kuelewa kuwa kuchangia damu ni kuokoa maisha ya wananchi wenzao.

Afisa huyo ameyataja makundi yenye uhitaji mkubwa wa damu kuwa ni pamoja na wanawake wajawazito,wanaojifungua na watoto walio chini ya miaka mitano.

Amesema mahitaji makubwa ya damu mengine yanaongezeka kutokana na mtindo wa maisha lakini pia ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara na majeruhi kuhitaji damu kwa wingi.

Mwamko mdogo umetajwa kuwa changamoto kubwa ya wananchi kushindwa kujitolea damu kutokana na kukosekana kwa elimu na mtizamo potofu kuhusiana na uchangiaji wa damu katika vituo maalum.

Malengo ya mpango wa Damu salama ni kufikisha Kiasi cha cha chupa laki tatu na elfu hamsini itakapofika mwaka 2015 na kwamba wana mikakati ya kuhakikisha elimu na hamasa inatolewa ili kurahisisha zoezi hilo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top