Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania,Klaus Peter Brandes
Suala la Uhuru wa vyombo habari
limetajwa kuwa mhimili mkubwa wa maendeleo na ukuaji wa demokrasia katika nchi yoyote ile ulimwenguni kwa ustawi wa watu wake.
Akizungumzia juu ya maadhimisho ya
miaka 50 ya Idhaa ya Kiswahili ya Redio Deutch Welle, Balozi wa Ujerumani hapa
nchini Klaus Peter Brandes amesema uhuru wa vyombo vya habari unahitajika ili
kuonesha ustawi na utashi wa ukuaji wa demokrasia ulimwenguni kote.
Hata hivyo balozi huyo amesema si lengo la Ujerumani kuingilia mambo ya
ndani ya nchi zingine wala vyombo vya habari vya ujerumani kama ilivyo kwa
radio Deutch Welle ambayo amedai ina uhuru wa kufanya kazi kwa mujibu wa sera
zake yenyewe.
Nao Mohamed Khelef na Mohamed Abdulrahman
ambao ni watangazaji wa Idhaa hiyo wamesema si kweli kwamba idhaa yao
inatangaza mambo mabaya kuhusu Afrika bali kuna vipindi vizuri kusaidia
maendeleo ya Afrika.
Naye mratibu wa Maandalizi ya
Maadhimisho ya Idhaa hiyo ANDREA SCHMIDT amesema wachagua Tanzania kuwa
mwenyeji wa sherehe za mwaka huu kutokana na uwingi wa wasikilizaji wa redio
hiyo na kuamini kuwa Ijumaa wiki hii itawakutanisha wadau mbalimbali za ukanda
wa Afrika Mashariki na kati.
0 comments:
Post a Comment