Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na maafisa mbalimbali wa ubalozi wa Tanzania Nchini Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa leo jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria hafla ya Utiaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete, kabla ya kurejea Dar es salaam leo, alikwenda Uganda kuhudhuria mazishi ya baba mzazi wa Rais Yoweri Kaguta Museveni, Mzee Amos Kaguta, aliyefariki siku ya Ijumaa na kuzikwa kijijini kwake
Balozi
wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram M. Biswaro akiwa na Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Naimi Aziz (kati) na Afisa
ubalozi Samwel Shelukindo wakipungia kumuaga Rais Kikwete wakati ndege
yake ikiondoka uwanjani hapo leo jioni ya Februari 24, 2013
PICHA NA IKULU
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment