MTU mmoja aliyejulikana kwa jina la Kotanida Petro (Umri wake haukupatikana) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mbagala kata ya Ilembo Mbeya Vijijini amefariki dunia akiwa shambani kwake baada ya kupigwa na radi jana majira ya saa 5 asubuhi.
Daktari katika Kituo cha Afya Ilembo ndugu Nelson George amekiri kupokea mwili wa marehemu Kotanida.
Naye Diwani wa kata ya Ilembo ndugu Patrick Zumba Mwasenga amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa marehemu alikuwa mke wa Mchungaji wa kanisa la Moraviani katika kijiji cha Mbagala kata ya Ilembo.
Mwili wa marehemu umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwao eneo la Ngwala Chunya kwa Mazishi.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani alipopigiwa simu kwa utibitisho alisema yupo nje ya kituo hivyo kuwa vigumu kuzungumzia suala hili.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment