Padre Evaristus Mushi
                                    
PADRI wa Kanisa Katoliki Mjini Zanzibar, Evaristus Mushi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akiegesha gari lake kando ya Kanisa Katoliki la Mtoni alipokwenda kuendesha ibada ya Jumapili katika kanisa hilo jana asubuhi. Matukio haya ya kihalifu yanavyozidi kuendelea kutokea ni jambo la kusikitisha sana kwa Zanziba. Jeshi la Polisi Mjini hapa halijatoa taarifa yoyote kuhusiana na kubainika kwa watu waliohusika katika mauaji hayo ya kinyama.
Wakati huo huo taarifa kutoka Ikulu zinasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa Padri Evarist Mushi wa Parokia ya Minara Miwili ya Kanisa Katoliki mjini Zanzibar, mauaji yaliyotokea Zanzibar.
Rais Kikwete anawapa pole nyingi na rambirambi za dhati ya moyo wangu Baba Askofu Augustino Shayo wa Jimbo Katoliki, Zanzibar na waumini wote wa Parokia ya Minara Miwili kwa msiba huo mkubwa uliowakuta.

Rais kikwete amemwambia Baba Askofu Shayo. ”Napenda kuwahakikishia kuwa tupo pamoja katika kuomboleza kifo cha Mpendwa Marehemu Padri Evarist Mushin a kuwa msiba huu ni wa kwetu sote.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Nimeligiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”
“Aidha, nimewaagiza Jeshi la Polisi washirikiane na vyombo vingine vya Usalama nchini na mashirika ya upepelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji haya.” Amesisitiza Rais Kikwete: “Nataka ukweli wake ujulikane ili kama kuna jambo lolote zaidi liweze kushughulikiwa na kukata mzizi wa fitina.”
Via: The Habari
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top