JULIANA SHONZA NA MTELA MWAMPAMBA WAJIUNGA NA CCM LEO.

Juliana Shonza akijitambulisha kwa wana CCM leo tarehe 12/2/2013, katika Makao Makuu ya CCM,mjini Dodoma
Mtela Mwampamba akijitambulisha kwa wana CCM,wakati wa sherehe za utambulisho wa  wajumbe wa kamati kuu ya CCM.

Mwenyekiti wa CCM-Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wapya  wa CCM,Juliana Shonza na Mtela Mwampamba,kushoto kwenye picha ni Makamu Mwenyekiti CCM-Bara ,Ndugu Philip Mangula na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahaman Kinana.
Mwenyekiti wa CCM-Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wa Dodoma wakati wa sherehe za kuipongeza Kamati Kuu iliyochaguliwa jana mjini Dodoma.

ZOEZI LA UPIGAJI KURA LILIVYOENDESHWA PICHANI

Monday, February 11, 2013



Wajumbe wa NEC wakiwa tayari kwa zoezi la kupiga kura


Maafisa wa chama wakiwa katika usimamizi wa shughuli nzima ya kupiga kura.

Makatibu wa NEC,Kutoka kushoto Zakia Meghji, Dk. Asha-Rose Migiro na  Mohamed Seif Khatib



Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akipiga kura kuchagua wajumbe wa Kamati Kuu ya  CCM

Makamu wa pili wa Rais, Zanzibar , Balozi Seif Idd na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mwigulu Lameck Nchemba wakipiga kura za wajumbe wa kamati kuu ya CCM,Taifa.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao chake cha siku mbili Februari 10 na 11, 2013 kilichofanyika mjini Dodoma, pamoja na mambo mengine kimeridhia uteuzi na kufanya uchaguzi wa Wajumbe 14 wa Kamati Kuu yake.

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imeridhia uteuzi wa Dokta Salim Ahmed Salim kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kupitia nafasi 10 za uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM. 

Wajumbe 14 waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni:-

Wajumbe wa Kamati Kuu - Bara
1. Ndugu Pindi Chana
2. Ndugu Adam Kimbisa
3. Ndugu William Lukuvi
4. Dokta Emmanuel Nchimbi
5. Ndugu Jerry Slaa
6. Profesa Anna Tibaijuka
7. Ndugu Stephen Wassira

Wajumbe wa Kamati Kuu - Zanzibar.
1. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
2. Ndugu Hussein Mwinyi
3. Profesa Makame Mbarawa Mnyaa
4. Dokta Salim Ahmed Salim
5. Ndugu Maua Daftari.
6. Ndugu Samia Suluhu Hassan
7. Ndugu Hadija H. Aboud

Imetolewa na:-          
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
12/02/2013
Chanzo: Mtandao wa CCM TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top