Walimu wote waliopewa ajira ya Ualimu Serikalini ambao majina yao yametangazwa katika tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI, wanatakiwa kuripoti tarehe 01 Machi 2013 kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri walikopangiwa kwa ajili yakupangiwa Vituo vya kazi. HAKUNA MABADILIKO YA VITUO VYA KAZI YATAKAYOFANYWA. Mwalimu anatakiwa kwenda na vyeti vyake halisi vya taaluma na cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake. Mwalimu ambaye hataripoti ifikapo tarehe 9 Machi 2013 atapoteza nafasi hiyo.

NB: WALIMU WALIOKWISHA AJIRIWA WARUDI KWA WAAJIRI WAO

Bofya hapa: Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top