Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Peramiho Jenistar Muhagama wakati wa mahafali ya saba ya kidato cha sita katika shule ya sekondari BAOBAB yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Amesema kuwa wazazi wengi hupenda kujiwekea bima ya afya na maisha na msisitizo mdogo katika suala la elimu jambo linalowafanya kuwa na watoto ambao hawawezi kumudu maisha yao na kushindwa kuwasaidia wazazi wao.
Akisoma risala ya shule kwa niaba ya mkuu wa shule mwalimu Vernus Lucas amesema kuwa shule ina mikakati ya kuwafanya wanafunzi wote wafaulu kwa kutumia wakati wa ziada kwa wanafunzi wenye kuhitaji uangalizi maalum. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment