Waislamu nchini wametakiwa kujikita katika maswala ya kiuchumi ili waweze kutoa Zaka ambayo ni nguzo muhimu ya  Uislamu. Kauli hiyo imetolewa na Amiri wa HAY-AT  Shekh Selemani Amrani
Kilemile  wakati wa sherehe fupi ya ugawaji wa zaka uliofanywa na Jumuiya ya Wataalamu wa kiislamu Tanzania( TAMPRO) wakishirikiana na jumuiya ya wanazuoni wa kiisalamu (HAY-AT) katika ukumbi wa hoteli ya LAMADA jijini Dar es salaam siku ya jumapili.
Shekh Kilemile  amesema kuwa  Zaka ni jambo muhimu katika maisha ya wanadamu kwa kuwa lengo lake ni  kuwasaidia mafakiri na masikini ili waweze kuendesha maisha yao.
Kwa upande wake Amiri wa baraza kuu la waislamu na shura ya Maimam Shekh Mussa Kundecha amesema tabia ya utoaji zaka itaweza kuondoa chuki inayoweza kujitokeza kati ya walionacho na wasionacho katika jamii
Naye katibu wa TAMPRO bwana PAZI MWINYIMVUA amesema kuwa kwa sasa waislamu wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ushirikiano jambo linalokwamisha juhudi za kuendeleza uislamu.
Katika hafla hiyo zaidi ya shilingi milioni 15 ziligawiwa kwa watu thelathini na moja  wakiwemo wajane na wanafuzi waliokwama kuendelea na masomo kwa kukosa ada.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top