Mkurugenzi wa Habari, Mawasiliano na Uenezi John Mnyika akiongea na Waandishi wa Habari,jijini Dar es Salaam
Katibu mkuu wa CHADEMA Dkt. Willibroad Slaa (kushoto) na Freeman Mbowe (kulia) akifafanua jambo katika mkutano mkuu wa chahicho jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanachama wa CHADEMA  wakifuatilia kwa makini kinachoendelea katika mkutano mkuu wa chama hicho.
 Mbunge wa Kawe Halima Mdee  akinukuu baadhi ya mambo muhimu wakati wa mkutano mkuu wa CHADEMA uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Chama cha demokrasia na maendeleo chadema kimeamua kutekeleza mpango wake wa kurudisha madaraka kwa wananchi na kugawa nchi katika majimbo ambapo sasa kimeigawa nchi katika majimbo kumi
Akielezea maamuzi ya kamati kuu kwa baraza kuu la chama hicho, mwenyekiti wa taifa Freeman Mbowe amesema kuwa mfumo wa serikali na nchi kwa sasa umekuwa na kasoro ambapo kikundi cha watu wachache hukaa Dar es salaam na kuamua kwa niaba ya wananchi.

Amesema Chama hicho sasa kimeamua kugawa nchi katika kanda kumi na kuhakikisha kuwa kila kanda inakuwa na maamuzi yake kwa  wanachama bila kutegemea maamuzi ya makao makuu ya chama.

Kuhusu sakata la gesi Mtwara, chama hicho kimesema kuwa kinaunga mkono msimamo wa wananchi na kuitaka serikali kuhakikisha kuwa masuala ya rasilimali za nchi yanaamuriwa na wananchi wenyewe ili kuondoa migogoro.

Mwenyekiti  huyo  amesema kuwa kamati kuu imetoa msimamo kuhusu mjadala wa katiba ambapo wamesema kuwa endapo katiba hiyo haitaleta mfumo wa serikali tatu na tume huru ya uchaguzi chadema itaongoza wananchi kupinga katiba hiyo.


Suala la Gesi Mtwara
Serikali imetakiwa kukaa chini na wananchi mkoani Mtwara ili kupunguza mgogoro unaofukuta ambapo wananchi wanapinga kusafirishwa kwa gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Mkurugenzi wa habari na UENEZI wa chama hicho John Mnyika amesema kuwa hali si shwari kutokana na wananchi kuwa nyuma kimaendeleo.
Bwana Mnyika amesema serikali inatakiwa kurekebisha kauli kwa kuwaita wananchi wa Mtwara na Lindi wachochezi badala yake wafunge safari na kukaa meza moja ya mazungumzo. 

PICHA NA GERVAS MWATEBELA TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top