Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael (LULU)
Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la LULU ambaye anatuhumiwa kwa kesi ya mauaji ya msanii Steven Kanumba hatimaye ameweza kupata nafasi ya kuweza kudhaminiwa katika mahakama kuu.
Msanii huyo anaweza kudhaminiwa endapo ataweza kutimiza masharti ambayo ni pamoja na Kuwa na wadhamini wawili wenye dhamana ya Shilingi milioni 20 kila mmoja, Kukabidhi pasi yake ya kusafiria kwa Msajili wa Mahakama,Kuripoti Mahakamani tarehe Mosi ya kila mwezi na kutosafiri nje ya nchi.
Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kupitia vifungu vya sheria na kuona kuwa, kwa kosa aliloshtakiwa sasa, msanii huyo anaweza kupata dhamana.
Hata hivyo, maafisa wawili wa Serikali (mahakama) wanaohusika na dhamana hawakuwepo mahakamani jambo lililokwamisha zoezi la dhamana hiyo. Kwa mantiki hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa LULU kupata dhamana kesho, Januari 29, 2013.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba April, 7 mwaka jana huko Sinza Vatican,jijini Dar es Salaam. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment