YANGA, TANZANIA PRISONS WAINGIZA MIL 101/-

Yanga na Tanzania Prisons zimeingiza mapato ya jumla ya sh. 101,016,000 katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara iliyofanyika jana (Januari 28 mwaka huu).
Mechi hiyo namba 94 ilichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-1. Watazamaji 17,946 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Watazamaji 16,158 kati ya hao walikata tiketi za sh. 5,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ni 98 waliokata tiketi za sh. 20,000.
Kila klabu imepata mgawo wa sh. 24,314,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 15,409,220.34. Asilimia 15 iliyokwenda kwenye uwanja baada ya kuondoa VAT na gharama za tiketi ni sh. 12,363,433.45.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 7,413,060.07, Kamati ya Ligi sh. 7,418,060.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,709,030.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,884,801.14.


TIGO YATANGAZA DROO YA SMART CARD
Kampuni ya Tigo Tanzania leo imetangaza kuwa itafanya droo kubwa ya promosheni yake ya Smartcard ambapo washindi 43 watabahatika kujishindia zawadi  mbali mbali  za kusisimua ikiwemo zawadi kuu ambayo ni tiketi ya bure ya kwenda na kurudi Madrid Uhispania pamoja na kulipiwa gharama zote za safari kwenda kutizama  mechi  ya soka kati ya Real Madrid na FC Barcelona.
Droo hii ambayo imepangwa kufanyika Januari 30, 2013 ni mwendelezo wa  droo za promosheni ya Smartcard ambazo zinaendelea kufanyika  kila mwezi, robo mwaka,  na kila mwaka. Smartcard promosheni ilizinduliwa Septemba 2012 hususan kwa ajili ya wateja wa Tigo ambao wanatumia smartphones.
Meneja  wa Tigo Internet Broadband, Bw.Tito Kafuma amesema Mbali na zawadi kuu ya droo hiyo, washindi 42  watabahatika  kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo tiketi 12 za sinema, tiketi 12 za klabu, tiketi 12 za kuangalia mechi za mpira kwenye klabu ya hapa nchini, vocha 3 za kununua bidhaa mbalimbali na vocha 3 za chakula cha jioni.
 Ameongeza kuwa mshindi wa kwanza  wa droo hii atajishindia tiketi ya bure ya kwenda na kurudi Madrid Uhispania na kulipiwa gharama zote za safari kwenda kuangalia  mechi  ya soka kati ya Real Madrid na FC Barcelona.

SELEMANI GALILE AJINOA DHIDI YA MBWANA ALLY
Bondia Selemani Galile yupo katika mazoezi ya maandalizi ya mpambano wake dhidi ya Mbwana Ally utakaofanyika February 2 katika ukumbi wa Lupinga Pub uliopo Yombo Dovya
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Galile amesema yupo fiti kwa mpambano huo kwani kwa sasa anasubiri siku ya siku tu ili aweze kufanikisha

Galile aliongeza kuwa siku hiyo itakuwa ni ya kwanza kwa wakazi wa Yombo Dovya kupata burudani ya masumbwi itakayosindikizwa na mabondia chipukizi

Antony Mathias atapambana na Abuu Mtambwe huku Ramadhani Mkundi akioneshana kazi na Kassim Gamboo na Mohamedi Zungu kutoka Zanzibar atapambana na Mbena Rajabu wa Dar

Siku hiyo ya Mpambano kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi atasambaza DVD zake mpya ikiwemo ya Marvin Hagler vs John Mugabi na Manny Pacuiao va Emanuel Juan Marquize ambazo atasambaza kwa mara ya kwanza katika ukumbi huo DVD hizo zinazoelekeza mbinu na shelia za masumbwi zenye uwezo wa kuwajengea uwezo mabondia na mashabiki kujua sheria mbalimbali za masumbwi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top