Mwenyekiti wa Baraza la Walaji (Watumiaji) wa huduma za usafiri wa anga akiongea na wanahabari katika ukumbi wa habari Maelezo Jijini Dar es Salaam.
Imeelezwa kuwa huduma za usafiri wa anga zinahitajika zaidi kutokana na kipato cha wananchi wengi kuyumba lakini gharama za maisha kupanda kila uchao.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa baraza la kutetea haki za watumiaji wa usafiri wa Anga Juma Fimbo wakati akielezea namna walivyopokea punguzo la nauli kutoka kampuni ya ndege ya Fast Jet.
Mwenyekiti huyo amesema utaratibu wa kutoa ofa ya punguzo la bei kwa abiria lipo ulimwenguni kote ili kuwasaidia walaji kupata usafiri kwa bei nafuu lakini wenye masharti ya kupunguza baadhi ya vitu.
Bwana Fimbo amesema hawajapoke malalamiko kutoka kwa watumiaji kudaiwa kutapeliwa na kampuni ya Fast Jet kwani kama kuna malalamiko wanatakiwa kuyasilisha rasmi kwa maandishi.
Amesema kutokana na mfumo wa uchumi huria imekuwa vigumu kwa serikali kupunguza gharama za usafiri kupitia kodi za wananchi kama ilivyowahi kutokea miaka ya nyuma wakati shirika la ndege Tanzania likifanya kazi kwa ufanisi.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top