Wakati Tanzania imeingia rasmi katika mfumo mpya
wa kurusha na kupokea matangazo ya Televisheni,baadhi ya wakazi wa jiji la Dar
es Salaam wamesema mfumo huo unakabiliwa na changamoto nyingi.
Katika mahojiano mahojiano maalum, baadhi ya
watumiaji hao ambao wamesema kuwa wananchi hawakujiandaa vilivyo kukabiliana na
changamoto.
Wananchi wamesema kuwa tatizo kubwa la baadhi ya
ving’amuzi ni kukatakata na kuganda kwa picha wakati matangazo yanaendelea kitu
ambacho wengi hawakutarajia.
Wananchi hao wamesema hata kama kuna chaneli za
bure lakini kuna changamoto kubwa ya gharama
za kununua ving’amuzi na vifaa vinavyoambatana katika kufanya kazi kwake.
Katika mitaa mbalimbali mwandishi ameshuhudia mamia
ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakihaha kusaka ving’amuzi katika maduka
yanayouza bidhaa hiyo muhimu kwa sasa
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment