Watanzania wametakiwa kuacha mawazo potofu juu ya
mgawanyo wa rasilimali zilipo nchini kwa sababu zinatumika kwa ajili ya
wananchi wote pasipo upendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa nishati na madini
Profesa Sospeter Mhongo wakati akitoa ufafanuzi kufuatia maandamano
yaliyofanyika mkoani Mtwara kwa madai kuwa ya gesi inayochimbwa mkoani humo kutowanufaisha
wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara.
Profesa Mhongo amesema maandamano kama hayo
yanaweza kuligawa taifa kwa sababu kila mkoa unatoa rasilimali zake ambazo
zinatumika na wananchi wa mikoa yote
bila kujali ukanda wa mikoa husika.
Waziri huyo amesema endapo wananchi wa kila mkoa wataandamana ni hatari kwa amani
na utulivu na ustawi wa wananchi.
Waziri Mhongo amewataka wanasiasa wanatakiwa kuangalia maslahi ya kiuchumi kwa Taifa badala ya kuwapotosha wananchi na
kusababisha mivutano isiyokuwa ya lazima
katika jamii.
Serikali imesema kuwa gesi asilia iliyogunduliwa
Mtwara imekuwa ikitumika kuzalisha umeme wa megawati 18 ambapo mikoa ya Lindi
na Mtwara hutumia kiasi cha Megawati 12 pekee.
Profesa Mhongo amesema serikali inaamini ujenzi wa
bomba la gesi asilia kutoka Mnazi Bay mpaka jijini Dar es Salaam utalinufaisha
zaidi taifa kwa kutumiwa katika viwanda,taasisi na matumizi ya kawaida
majumbani.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment