Wanaharakati na Watetezi wa haki za binadamu wametakiwa kuwa
waangalifu wanapowajibika kutokana na vitendo vya ukatili ambavyo
wamekuwa wakifanyiwa katika siku za karibuni.
 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa usalama wa miaka mitano, Mratibu Onesmo Rugurumwa amesema mpango huo utawasaidia pindi wanaharakati watakapokuwa wanafanya kazi hizo.
Mratibu huyo amesema kuwa mpango mkakati huo umelenga katika
kuhakikisha watetezi haki za binadamu wanalindwa katika mazingira yao ya kazi.

Naye Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Dakta Hellen Kijo Bisimba amesema suala la ulinzi na usalama ni muhimu kwa wanaharakati na kupunguza vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Mkurugenzi huyo amesema vitendo vya kujichukulia sheria mikononi vimekuwa vikiongezeka kila siku ambapo pia amegusia kuwa imefikia hatua hata walinda amani wamekuwa wakivamiwa na kupigwa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top