Rais Jakaya Mrisho Kikwete |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Zurich,
Uswis kwa ajili ya
ziara ya kikazi ya siku 3 ambapo pamoja na mambo mengine anahudhuria mkutano wa Dunia kuhusu Uchumi
Mara baada ya kuwasili Zurich, Rais ametembelea makao makuu ya ofisi za shirikisho la soka duniani, FIFA na kupokelewa na Rais wa FIFA Bw. Joseph Sepp Blatter.
Rais Kikwete ametumia nafasi hiyo kumshukuru Bw. Blatter kwa kuinua kiwango cha soka barani Afrika na Tanzania kwa ujumla ambapo misaada mingi ya kifedha na kiufundi imepatikana kwa ajili ya kuendeleza soka nchini.
Tanzania ni mwanachama wa FIFA kupitia, Chama cha Mpira Tanzania-Tanzania Football Federation (TFF).
Kama shirikisho mama la mpira duniani, FIFA ina jukumu la kukuza na
kuendeleza soka duniani kote na hivyo imeweka mikakati na programu
kadhaa za kufanikisha malengo yake ambapo kiasi cha dola za Marekani laki mbili na nusu kwa kila mwanachama, Tanzania ikiwemo.
Mbali na hiyo kila mwanachama wa FIFA anaweza kupata msaada wa dola laki nne kila baada ya miaka 4, na msaada huu uliongezwa hadi kufikia dola laki tano tangu mwaka 2010 Kwa ajili ya malengo ya muda mrefu wa kuendeleza na kuinua soka kwa nchi mwanachama.
Hii leo Rais Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mikutano
kadhaa inayoendelea mjini Davos akiwa ni mtoa mada kuhusu Sekta za Maji, Kilimo na Miundombinu
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment