Zitto Kabwe |
Imeelezwa kuwa sheria ya mawasiliano na madini
haijaweza kutumika
kuwanufaisha Watanzania kutokana na serikali kushindwa kutunga kanuni kwa ajili ya utekelezaji wake.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma Zitto Kabwe wakati wa mahojiano maalum mara baada ya kupitia taarifa iliyotolewa na TCRA.
Mwenyekiti huyo amesema ilitolewa miaka mitatu kwa waziri kutunga
kanuni ya sheria ya mawasiliano kwa ajili ya utekelezaji wake lakini
bado miezi sita kabla ya kumalizika kwa kipindi hicho.
Amesema kuwa utekelezaji wa sheria hiyo ungewezesha kuingia katika soko la hisa la Dar es Salaam hivyo kuwanufaisha Watanzania.
Mwenyekiti huyo amesema kanuni zikiundwa na kulazimisha makampuni ya simu kuingia kwenye soko la hisa itakuwa vigumu kukwepa kodi kwani hesabu zake zitakuwa wazi hivyo ni rahisi kufuatilia.
Naye Mkurugenzi wa TCRA Profesa John Nkoma amesema wanafuata sheria katika utekelezaji wake kisha watawasiliana na makampuni husika ili kujua sababu ya kutojiorodhesha katika soko la Hisa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment