![]() |
Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani la Tanzania, Joyce Ndalichako. |
Kuanzia tarehe 01 Machi 2013 hadi tarehe 31 Machi 2013 waombaji watajisajili kwa ada ya shilingi 50,000/= kwa CSEE na 30,000/= kwa QT (ada pamoja na faini).
Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti: www.necta.go.tz. ya Baraza la Mitihani la Tanzania. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) watakazotumia kujisajili. Hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kupata namba rejea kutoka katika kituo anachokusudia kufanyia mtihani. Wakuu wote wa vituo nchini wamekabidhiwa namba rejea hizo tayari kwa kuzigawa kwa watahiniwa tarajali bila malipo.
LIMETOLEWA NA:
KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
Via NECTA
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment