Imeelezwa kuwa misingi
ya haki za binadamu inaweza kutekelezwa endapo tu nchi husika itafuata mfumo wa
utawala bora ambao utakuwa unatoa haki kwa kila mwananchi kushiriki kikamilifu
katika shughuli za uzalishaji mali.
Kauli hiyo imetolewa
na mhadhiri wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, James jesse wakati
wa mkutano wa kufanya tathmini mapendekezo yaliyotolewa wadau kuhusiana na masuala
mbalimbali yanayohusu haki za binadamu.
Bwana Jesse amekiri
bado kuna changamoto katika suala la kumiliki mali hususan ardhi kwa mwaanchi wa
kawaida hivyo ameitaka serikali kuwashirikisha wananchi katika masuala yote ya
kumiliki rasilimali za taifa kwani hilo ni jukumu la serikali yoyote duniani.
Katika hatua nyingine
mhadhiri huyo wa chuo kikuu cha dare s salaam, amekanusha kuwa misingi ya haki
za binadamu haiwezi kutekelezeka kwani kuna nchi nyingi ambazo zimeweza
kuheshimu na kutekeleza kwa vitendo haki za binadamu kwa wananchi wake.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment