SALUM HARUNA MSONGELE NI MMOJA WA WAFANYAKAZI WA WALIOACHISHWA KAZI KINYUME CHA SHERIA AMEITUMIKIA KAMPUNI YA KOBIL TANZANIA HIYO KWA MIAKA 11 |
RAMADHANI KIDAWEMBA PIA ALIKUWA MFANYAKAZI WA KOBIL TANZANIA KWA MIAKA 10 |
CHRISTINA PAUL KIBOMA |
Wakiongea katika mahojiano maalum wawakilishi wa
wafanyakazi hao wamedai waliachishwa kazi ghafla kwa madai ya kampuni yao
kuyumba na kushindwa kujiendesha hivyo kuamua kupunguza wafanyakazi 12 kati ya 43.
Wawakilishi hao Christina Paul Kiboma,Salum Haruna
Msongele na Ramadhani Kidawemba wamesema kuwa wanachopinga ni kunyanyaswa na
kuachishwa kazi kinyume cha sheria pasipo mawasiliano ya awali na kuamriwa
kuondoka ndani ya dakika 10 tu.
Baadhi ya wafanyakazi waliopunguzwa kazini walinyang’anywa
vifaa binafsi na akaunti zao kufungwa mara
baada ya kuachishwa kazi hivyo kuwaomba wanaharakati za binadamu
kuingilia kati na kuwatetea na kunyanyaswa uongozi wa kampuni hiyo.
Jitihada za kumpata kaimu mkurugenzi wa kampuni hiyo
bwana Paul Mkato zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment