Vijana wametakiwa kujitambua kuwa wao ndio nguvu kazi ya taifa na kutumia wao mwingi katika shughuli za kujileta maendeleo wao wenyewe na taifa kwa ujumla.
mkurugenzi wa kampuni ya maboma bwana Simon Ndiganya amesema kuongezeka kwa vitendo viovu yakiwemo matukio ya wizi kunasasababishwa na vijana wengi kushindwa kujitambua na kutumia nguvu kazi yao kwa uzalishaji

Amesema endapo vijana nchini watatambua fursa walizo nazo na kuzitumia ipasavyo,vitendo hivyo viovu vitapungua kwa kiasi kikubwa na maisha kwa ujumla yataimarika
Bwana Maboma amesema tofauti na miaka ya nyuma,hivi sasa kuna kampuni nyingi ambazo zinatoa mafunzo ya stadi za maisha kama vile ujasiriamali,na kuwataka vijana kutumia fursa hizo kupata stadi ili waweze kujiajiri wenyewe
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top