Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bwana Victor Nkya |
Imeeelezwa kwamba gharama za mwingiliano mawasiliano ya simu kutoka mtandao mmoja kwenda mtandao mwingine zinatakiwa kupitiwa
upya ili kumpunguzia mzigo kwa wananchi.
Akiongea wakati wa
mjadala kuhusiana na gharama hizo Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Victor
Nkya amesema utafiti unaonesha kuwa gharama zinaweza kupunguzwa zaidi na
kuwanufaisha watumiaji wa simu za mikononi.
Bwana Nkya amesema baada ya utafiti TCRA imeona kwamba
mwananchi aweza kutumia shilingi 34.9 badala ya shilingi 113 ambazo zinatumika katika mitandao ya simu kwa
hivi sasa.
Hata hivyo kwa upande wa wadau hususani wawakilishi wa kampuni zinazotoa huduma za simu
wameonekana kutofautiana kimsimamo kwani wengi wanaonekana kutounga mkono wazo
la kushusha gharama kuanzia mwezi Machi mwaka huu.
Wawakilishi hao wamesema hofu yao kubwa ni kushindwa kumudu gharama kubwa za uendeshaji hivyo huenda
wakajiendesha kwa hasara na hatimaye kufilisika.
Kwa upande wa wananchi wamesema kama pendekezo hilo litapitishwa
litawapa ahueni kwani wamekuwa wakiingia gharama kubwa wanapowasiliana kutoka Mtandao
mmoja hadi mwingine.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment