Waziri Mkuu Mizengo Pinda

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema kuwa fedha zote ambazo wenyeviti wa vitongoji wanaidai Serikali kama posho ya usimamizi wa zoezi la sensa ya watu na  makazi  zitalipwa hivi karibuni.

Waziri mkuu Pinda ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Kibaoni kwenye uwanja wa shule ya msingi Kakuni ambako pia ni kijijini kwao akiwa katika siku ya kumi ya ziara yake jimboni kwake Katavi

Waziri Mkuu amesema wenyeviti wote waliofanya kazi kwa siku saba na wale ambao maeneo yao yaliongezwa siku za ziada watalipwa kwa sababu fedha zimeshapatikana.

Amesema Serikali imeshafanya hesabu zake na kubaini jumla ya shilingi bilioni 3.1 zinahitajika kwa ajili ya malipo hayo

Zoezi la sensa ya watu na makazi lilifanyika nchini kote mwezi Augusti mwaka huu kwa lengo la kutambua idadi halisi ya watu waliolala nchini usiku wa kuamkia siku ya sensa ili kuwezesha upangaji wa mikakati mbalimbali ya maendeleo
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top