Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amepiga marufuku halmashauri kulazimisha mabasi ya mikoani kuingia katika vituo vyao vya mabasi na kulipa ushuru hata kama hayashushi wala kupakia abiria.

Dk Mwakyembe ametoa kauli hiyo  alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam

Lengo la ziara hiyo lilikuwa kujionea utendaji kazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na Kikosi cha Usalama Barabarani, katika kudhibiti upandaji holela wa nauli wakati wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Katika kutekeleza agizo hilo, Dk Mwakyembe ameagiza vizuizi vyote vilivyoanzishwa na halmashauri kwenye vituo vilivyopo katika barabara kubwa kwa ajili ya kukusanya ushuru, viondolewe, 

Amesema kitendo hicho kinawapotezea abiria muda wa kufika wanakokwenda bila sababu za msingi, na kuvitaja  vituo vinavyolalamikiwa kwa usumbufu huo kuwa ni Mafinga, Kibaigwa, Nzega, Kibaha na vingine.


Akizungumzia hali ya usafiri katika kipindi hiki  cha sikukuu hizo za Krismasi na Mwaka mpya, Waziri Mwakyembe amesema hali aliyoikuta kituoni hapo inaridhisha kwa kuwa abiria wote kwenye mabasi walikuwa wamepata tiketi kwa bei elekezi ya Sumatra.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top