Watanzania wametakiwa kuimarisha umoja amani na mshikamano kwa mustakabali mwema wa Taifa katika siku za usoni na kuepuka vurugu ambazo zaweza kusababisha migogoro katika jamii.
Hayo yamesema na Askofu Godfrey Malasi akizungumzia maandalizi ya Ibada ya mkesha wa Mwaka mpya itakayofanyika uwanja wa Taifa Desemba 31 mwaka huu.
Askofu huyo amesema kuwa  suala la amani ya utulivu ni suala linalotakiwa kupewa kipaumbele na kama Watanzania watakataa kutumiwa vibaya basi Tanzania itazidi kuwa imara katika Nyanja zote.
Naye Mchungaji kutoka Zimbabwe Dakta Charles Mugalili amesema waafrika wanatakiwa kuombea ya amani ya nchi zao na kupunguza migogoro inayoendelea hapa barani Afrika.
Wakati Ibadaya mkesha wa mwaka mpya kuombea Taifa amani ikitaraji kufanyika, huko visiwani Zanzibar imeripotiwa kuwa Paroko wa Kanisa Katoliki Ambrose Mkenda alipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya akitoka kanisani juzi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top