Sehemu ya Makumbusho ya Taifa |
Wito
umetolewa kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea makumbusho
yanayohifadhi historia na utamaduni wetu na kuachana na dhana potofu ya kudhani maeneo
hayo ni kwa ajili ya vitu vilivyoharibika.
Afisa Elimu
wa Makumbusho ya Taifa Mawazo Ramadhani amesema licha ya hamasa kuongezeka siku
za karibuni lakini watanzania wengi
wamekuwa hawaoni umuhimu wa kutembelea maeneo Makumbusho na kujua historia na
vitu mbalimbali.
Afisa Elimu
huyo amesema kwa sasa utalii wa kiutamaduni
ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza mila na desturi ya jamii ya Watanzania
na kurithisha kizazi kimoja hadi kingine.
Bwana
Ramadhani amesema mfumo wa Elimu unatakiwa kulenga kwa kiasi kikubwa katika
kuendeleza Utalii wa ndani kwa watoto na vijana ambao wataweza kujua umuhimu wa
sekta hiyo katika jamii.
Imeelezwa
taasisi za elimu kama shule na vyuo ndiyo huongoza kutembelea katika makumbusho
ya Taifa,wakati siku za Wikiendi na sikukuu ndiyo hupokea watalii wengi wa
ndani ya nchi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment