Madaktari wakiwa katika tafakari |
Baraza
lilipitia malalamiko yote na limetoa adhabu stahiki kwa kila daktari
aliyethibitishwa kushiriki katika mgomo huo.
Adhabu hizo zilikuwa katika makundi yafuatayo; onyo, onyo kali na kusimamishwa
udaktari kwa muda wa kati ya mwezi mmoja na miezi sita.Vile vile kuna Madaktari
ambao hawakuwa na hatia ya kushiriki katika mgomo na hivyo walifutiwa mashtaka.
MCHANGANUO WA ADHABU
- Waliofutiwa mashitaka madaktari 49
- Waliopewa onyo madaktari 223
- Waliopewa onyo kali madaktari 66
- Kusimamishwa kwa muda madaktari 30
- Mashitaka yaliyoahirishwa kutokana na wahusika kuhitaji ushauri wa kisheria madaktari 4
- Mashitaka yasiyosikilizwa kutokana na wahusika kutofika walipoitwa na Baraza madaktari 22
Wizara
inakamilisha taratibu za kinidhamu kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma kwa
Madaktari wote waajiriwa ambao walipatikana na hatia mbele ya Baraza la
Madaktari. Wizara pia imeridhia kuwapa
Madaktari waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo fursa nyingine ya kuendelea na
mafunzo hayo katika hospitali za Umma walizokuwepo kabla ya kuondolewa. Hata hivyo fursa hii haitawahusu Madaktari
wote waliopewa adhabu za kusimamishwa na Baraza la Madaktari, hadi hapo
watakapomaliza kutumikia adhabu zao.
HITIMISHO
Kwa
taarifa hii madaktari wote waliofutiwa mashtaka na wale waliopewa onyo na onyo
kali wanatakiwa kuwasilisha kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
barua kutoka kwa msajili wa Baraza la Madaktari ikithibitisha kurejeshewa
usajili na kuruhusiwa kuendelea na
mafunzo kwa vitendo. Vile vile madaktari waajiriwa(Registrar) wanatakiwa pia kuripoti
kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya ili kupewa barua zao kulingana na Adhabu
walizopewa. Barua hizi zitatolewa kuanzia tarehe 2 Januari, 2013.Madaktari wote
walio katika mafunzo kwa vitendo wanatakiwa kuanza kazi katika vituo vyao vya awali
ifikapo tarehe 14 Januari, 2013.Hakuna muda utakaoongezwa kwa kipindi
kilichobakia cha mafunzo kwa vitendo. Kwa wale wote waliopewa adhabu
wataanza kutumikia adhabu hizo kuanzia tarehe ya adhabu hiyo ilivyotolewa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment