Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Charles Kenyela
Kamanda wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam Charles Kenyela amesema watu wawili wameuawa katika matukio tofauti katika manispaa hiyo.
Kamanda Kenyela amewataka Wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi pindi wanapowakamata watu wanaowatuhumu kuwaibia ama kuvunja sheria.
Kamanda Kenyela amesema tukio la kwanza limetokea eneo la Magomeni magomeni makuti eneo la Somanga kijana mwenye miaka kati ya 25 – 30 ameuwawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za kutaka kuiba pikipiki.
Maiti ya kijana huyo ambaye jina lake halikuweza kutambuliwa mara moja imehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala ambapo kamanda Kenyela amewataka wananchi waliopotelewa na ndugu yao wafike hospitalini hapo ili kumtambua.
Kamanda Kenyela amesema Katika tukio jingine limetokea hoteli ya  SeaCliff ambapo raia mmoja wa Bulgaria mfanyakazi wa Hoteli ya Kilimanjaro amenyogwa na kukatwa miguu.
Hata hivyo kamanda huyo amesema ukiacha matukio  hayo mawili yaliyojitokeza hali ya mkoa wake ipo shwari na polisi inajipanga kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya.



 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top