Mfumo hafifu
wa mawasiliano baina ya bodi ya mikopo
ya elimu juu na wanafunzi wa vyuo vikuu umetajwa kuwa chanzo cha migomo na
migogoro isiyokwisha katika taasisi za elimu hapa nchini.
Mtafiti
kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kileo amesema kuwa bodi ya mikopo imekuwa
ikitoa taarifa ambazo hazitoshelezi hivyo waombaji wa mikopo kutopata taarifa za kina
kupitia njia mbalimbali za chuo.
Bwana Kileo
amesema kuwa matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba teknolojia ya habari na
mawasiliano bado haijawanufaisha wanafunzi kwa kiasi kikubwa na kuwalazimisha
kuwasiliana na bodi ana kwa ana badala ya kutumia mtandao.
Mtafiti huyo
ameishauri bodi ya mikopo kuhakikisha inapunguza urasimu katika kushughulikia
masuala ya mikopo kwa wanafunzi pia
taarifa zote muhimu ziwekwe kwenye mtandao kuepusha usumbufu usio wa lazima.
Katika miaka
ya hivi karibuni migomo ya wanafunzi imekuwa ikitokea mara kwa mara kutokana na
sababu mbalimbali ikiwemo malalamiko ya kutopatiwa mikopo kwa wakati na mchakato
wa upangaji madaraja ya mikopo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment