Wanataaluma wa chuo kikuu cha Dar es salaam wameandaa
kongamano kutathmini matumizi ya rasilimali za taifa pamoja na mustakabali wa Taifa kwa kipindi cha miaka 50
ijayo
Mwenyekiti wa jumuiya ya wanataaluma
hao [UDASA] DKT FRANCIS MICHAEL amesema wameamua kufanya kongamano hilo
kutokana na mahitaji makubwa ya wananchi kutaka ufanyike upembuzi yakinifu kuhusu rasirimali za taifa
Baadhi ya mambo watakayojadili ni
kuhusiana na amani na utulivu,mfumo wa elimu ya Tanzania kwa miaka 50 iliyopita
na mustakabali wa taifa katika miaka 50 ijayo.
Aidha DKT MICHAEL ameongeza kuwa
majadiliano juu ya mambo muhimu ya nchi yatahusisha wataalamu wa chuo kikuu cha
Dar es salaam, viongozi mbalimbali pamoja
na wananchi wa kawaida.
Kongamano hilo jinatarajiwa kufanyika
disemba 9 mwaka huu 12 katika ukumbi wa Nkrumah mara tu baada maadhimisho ya sikukuu ya uhuru wa Tanganyika.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment