Shirikisho la mpira wa mguu Tanzania (TFF) limetoa
pongezi kwa timu za Tanzania baada ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano
ya chalenji inayoshirikisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na kati .
Rais wa shirikisho
hilo leodgar Tenga.ametoa pongezi kwa
Kilimanjaro stars na Zanzibar Heroes kwa
hatua waliofikia nakusema kuwa nia yao ni kufanya vizuri zaidi.
Rais huyo amesema kuwa mchezo walioonesha wawakilishi wa Tanzania
umetoa faraja kwa medani ya soka hapa nchini ikiashiria mwanzo wa kufanya
vizuri katika michuano mingine ya kimataifa.
Timu za Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes zimetinga
hatua hiyo kwa kuziondosha timu za Rwanda na Burundi katika mechi za Robo
fainali katika michuano hiyo itakayofikia kilele chake hapo Desemba 8 mwaka
huu.
Katika hatua nyingine Rais Tenga amewapongeza vijana chini ya miaka 17 na pia kuwashauri wadau
kuwalea vizuri kuwalea vijana hao kwani wanaweza kuwa hazina ya taifa katika
siku za usoni.
Licha ya timu hiyo kutolewa katika michuano ya kuwania
fainali za Afrika na Congo Brazzavile kwa jumla ya magoli 2 – 1 Rais amesema
timu hiyo inahitaji kuendelezwa na ametoa wito kwa wadau kuzisaidia timu za
vijana na wanawake kwani timu hizo hazina wadhamini.
Timu za vijana wanawake zimekuwa zikicheza katika
mazingira magumu hivyo kuhitajika msukumo wa kutosha ili ziweze kupiga hatua
endelevu.
0 comments:
Post a Comment