Wakuu wa nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki wameahirisha kufanya maamuzi juu ya maombi ya nchi
za Sudani Kusini na Somalia kujiunga na jumuiya hiyo ya kiuchumi yenye
wanachama watano.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa mwishoni mwa mkutano huo,
imeuelekeza Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo ambao ni chombo cha kufanya maamuzi cha kufanya
majadiliano zaidi na nchi hiyo mpya kabisa duniani na kuzingatia pia ripoti ya
kamati ya tathmini juu ya suala hilo.Maamuzi hayo yalifikiwa baada ya viongozi hao wa nchi wanachama kupokea
taarifa ya maendelea ya maombi ya Sudani Kusini, kujiunga na EAC.
Sababu za kuahirishwa kukubaliwa kwa maombi ya nchi hizo mbili
hazijafahamika.
Sudani Kusini iliomba kujiunga na EAC miezi michache tu baada ya
kupata uhuru wake mwaka jana wakati Somalia iliwasilisha maombi yake Februari,
2012. Aprili, mwaka huu, viogozi wa kanda hiyo walipokutana mjini
Bujumbura, Burundi, waliahirisha kufanyia maamuzi maombi ya Sudani Kusini, hadi
Novemba.
Kuhusu ombi la Somalia, mkutano wa
wakuu hao pia umeuelekeza Mkutano wa
Baraza la Mawaziri wa kuanza mchakato wa
uhakiki wa maombi hayo na kuwasilisha taarifa katika mkutano wa 15 wa wakuu
hao.
0 comments:
Post a Comment