Picha ya kocha mkuu anayetaraji kuingia makubaliano na Simba ya Dar es Salaam ambapo mwenyekiti wa simba Ismail Aden Rage amethibitisha kuanza mazungumzo na kocha huyo.(Picha kwa hisani kwa mitandao)

KOCHA wa zamani wa Akademi ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Club Africain ya Tunisia, Patrick Liewig ndiye atakayerithi mikoba ya Mserbia, Milovan Cirkovick katika klabu ya Simba.

Bwana Rage amesema kocha Liewig atatua nchini baada ya Krisimasi kuja kuanza kazi. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top