Muonekano wa ghorofa hilo alipojirusha mwanafunzi huyo.
Mwanafunzi
mmoja wa ChuoKikuu Dodoma – UDOM aliyefahamika kwa jina la KAMUGISHA
S/O ISACK, Miaka 24,Mhaya, Mwaka wa Tatu, Kitivo cha Sayansi ya Jamii
(Social Science) anayeishi Block Namba 11, chumba Namba 62, alijitupa
kutoka ghorofa ya pili hadi chini na kusababisha majeraha sehemu za
mdomoni, shingoni na paji la uso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amesema tukio hili limetokea
terehe 18/03/2014 majira ya 20:15 huko maeneo ya chuo kikuu cha Dodoma
manispaa na Mkoa wa Dodoma.
Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali
umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ulevi. Majeruhi alilazwa katika
hospitali ya UDOM na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na
kuruhusiwa tarehe 20/03/2014 baada ya kuonekana hali yake inaendelea
kuimarika.
Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani baada ya kukamilisha taratibu zote kujibu
shitaka la kujaribu kujiua.
0 comments:
Post a Comment