Hakuna mtu asifahamu hivi sasa kua viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wamekabwa roho na viongozi wenzao wa Bara kama vile Mchawi kuambiwa zamu yako imefika atowe mtoto wake.

 Lakini wajuwe tu kuwa hii Zanzibar si mali ya CCM, ni mali ya wananchi wote wa visiwa hivi vya Unguja na Pemba.

Chakushitusha na kuwashangaza wananchi wa Zanzibar hivi sasa, ni kuona CCM wanahaha kutaka kuidalali Zanzibar kama vile ni rasilimali yao.

Taharuki iliyowafanya wananchi wa Zanzibar waanze kua-Alart hivi sasa ni ,kikao cha dharura cha juzi kilichoongozwa na Mizengo Pinda na habari zake kuvuja mitaani.

Sindikizo la kikao hicho ni msimamo mwengine wa pamoja wa CCM kutaka nchi iwe moja tu na zitakazo baki ziwe na mawaziri wakuu.

Hili tayari badhi ya wahafidhina wameshalikubali niwachache tu walio pinga shingo upande, hii ni kutokana na Kusema Pinda kuwa kubadilisha katiba ya Zanzibar kifungu cha 10 kusema kua Zanzibar ni nchi na raisi wa Zanzibar kugawa mikoa nikuvunja katiba ya Muungano .

Sasa ili kuweka usawa wa katiba ya Muungano ijayo ni lazima katiba ya Zanzibar ifute kifungu hiki na isijitambulishe kuwa nchi iwe moja ya Tanzania na zitakazobaki zitakua na mawaziri wa kuu tu kama mfumo wa serekali mbili ukibadilika.

Kwa hio Wazanzibar hii sasa imekuwa si kitu chakupuuza ni (sirius case) hawa jamaa zetu CCM/SMZ tukisema kila kitu tuwachie tu basi wanaweza kuidalali Zanzibar na watu wake.

Hivi sasa wameshaonyesha kuwa na woga wa viticho vya kugawanywa kwa kutishwa eti vitega uchumi vyao walivyo wekeza viongozi Tanzania Bara vinaweza kuathirika ikiwa kutakua na 3, si mumemuona hata Kificho anavyoazirika sasa na kubabaika kama vile akifukuzwa ccm ndio hana maisha tena?.

Wengine katika kikao wamefika mbali na kutoa hoja zisizo "make sense" eti nibora kuwa na Serekali moja kwa kua Serekali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar SUK muna Ma-cuf na inaongozwa na Maalim Seif.

Sasa kwani hii ni kumkomoa Maalim Seif kua ikiwa Zanzibar haitokua nchi na Serekali ya Umoja wa Kitaifa SUK itavunjika ndio kumkomoa Maalim au ni kuwakomowa Wazanzibar wote na kizazi chetu cha Badaye.

Chuki hizi nyingine nizaujinga, ccm hivi sasa wanahaha na ni sawa na Mchawi anae daiwa mtoto kwa hiyo kama wananchi wa Zanzibar hatukua kitu kimoja kwa kupinga kwa nguvu zetu zote, basi tusubiri kuja kulaumiana na itakua tayari ndugu zetu wamesha tuza na Zanzibar imekwenda.

Mumemsikia Mbunge wa Magomeni Chombo tutoke kwenye Serekali mbili na tuingie kwenye Serekali 1 ili udugu wetu wa damu ukuwe zaidi na dungane zaidi.

Haya ndio mawazo yao akina Chombo na ccm wenzake Zanzibar.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top