Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imesema itaboresha zaidi mfumo wa utumiaji wa mashine za elektroniki katika utoaji risiti kwa wafanyabiashara wote.

Akizindua awamu ya pili ya mfumo huo,Naibu Kamishina mkuu wa mamlaka hayo Bwana Rashed Bade amesema katika awamu ya kwanza walikumbana na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa elimu na wasambazaji vifaa wachache.

Kamishina huyo amesema wamelenga kuongeza idadi ya watengenezaji kutoka wane hadi wanane ili kuongeza ufanisi wa kazi hivyo walaji kunufaika zaidi na teknolojia hiyo.

Katika hatua nyingine Bwana Bade amewataka wafanyabiashara kujiunga kwa haraka katika mfumo huo ili kupata  faida ikiwemo kupata taarifa sahihi kwa haraka zaidi ikiwemo kujua bidhaa zilizouzwa na ambazo hazikuuzwa.

Nao wafanyabiashara wamekiri kuwa utaratibu wa mfumo  huo ni mzuri lakini mamlaka ya mapato Tanzania inahitajika kutoa elimu zaidi kwa wafanya biashara ili wapate hamasa ya kutumia risiti zake.

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imepewa changamoto ya kutoa elimu zaidi kwa wafanyabiashara ili waweze kupata uelewa juu ya utumiaji wa risiti za elektroniki mfumo ambao umetajwa kurahisisha katika utunzaji wa kumbukumbu na kuisaidia serikali kupata kodi yake kwa usahihi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top